Manchester United waanika bei ya Schwensteiger kwa atakayemhitaji
Klabu ya Man United wameweka bei ya kuanzia kwa atakayetaka
kumnunua kiungo wao Bastian Schwensteiger ambayo ni pauni mil 2.
Nyota huyo aliambiwa kwamba klabu haina mpango nae na amekua akilazimika kufanya mazoezi na kikosi cha vijana tangu ujio wa kocha Jose Mourinho.
Gazeti la kijerumani, Bild limedai United wako tayari kumuuza Schwensteiger kwa kiasi kisichopungua pauni mi 2 ikiwa ni mwaka tangu awasili kutokea Bayern Munich kwa pauni mil 7.
Juventus wameonekana kuhitaji huduma ya mkongwe huyo ikiwa ni harakati za kuziba pengo la Paul Pogba huku wakijitahidi kumleta Blaise Matuidi kwanza.
Manchester United waanika bei ya Schwensteiger kwa atakayemhitaji
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 24, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 24, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment