Propellerads

Mourinho afunguka kwanini aliamua kurejea Premier League na kukacha Italia na Hispania



Kocha Mreno, Jose Mourinho amefunguka kwamba angeweza
kurejea Hispania au Italia kabla ya kukubali kufundisha Manchester United, na amefafanua kwanini hakukubali.

Kocha huyo alitimuliwa Chelsea mwezi Disemba mwaka jana baada ya Blues kuporomoka kiwango na kujikuta wakifikia mpaka  nafasi ya 16.

Sasa Mourinho amefunguka kua alikua na ofa La Liga na Serie A lakini alipendelea zaidi kukaa England.

"Nilikua na nafasi ya kwenda Italy au Hispania lakini Premier League ni special" aliiambia  Gazetta dello Sport.

"Katika baadhi ya nchi, vilabu vikubwa daima vinataka kua vizuri na kuviacha vidogo nyuma,"

"England nafasi inatokea. Hapa wanataka vilabu vyote kwenye ligi kua na ushindani."

Mourinho na kikosi chake watapambana na Hull City katika Premier League Jumamosi.
Mourinho afunguka kwanini aliamua kurejea Premier League na kukacha Italia na Hispania Mourinho afunguka kwanini aliamua kurejea Premier League na kukacha Italia na Hispania Reviewed by Steve on Tuesday, August 23, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.