Propellerads

TP Mazembe mabingwa Afrika

                 


TP Mazembe wamechukua ubingwa wa Afrika baada ya kuitwanga
USM Alger ya Algeria kwa mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Lubumbashi, DR Congo, imefanya Mazembe kubeba ubingwa kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya ushindi wa 2-1 ikiwa ugenini Algers.
Mashujaa wa Mazembe katika mechi ya leo walikuwa ni Mtanzania, Mbwana Samatta  aliyefunga bao la kwanza kabla raia wa Ivory Coast, Roger Assale akifunga la pili akimalizia kazi nzuri ya Samatta.

             

Samatta ndiye alianza kufunga bao la kwanza katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa pelnalti likiwa ni la pili kwake katika michezo miwili ya fainali kwa kuwa alifunga moja waliposhinda 2-1 ugenini.

Bao hilo ni la saba kwa Samatta, bao hilo linamfanya kujumuika na Bakry 'Al Medina' Babiker raia wa Sudan anayekipiga Al Merrikh. Hao sasa ndiyo wanakuwa wafungaji bora.

Assale ndiye alimaliza kabisa juhudi za Walgeria hao ambao walionekana kusaka angalau bao moja la ugenini baada ya kufunga bao katika dakika za majeruhi kwa kuugusa tu baada ya pasi saafi ya Samatta akiwa ameuwahi mpira mrefu na kuongoza counter attack iliyomaliza kazi.
TP Mazembe mabingwa Afrika TP Mazembe mabingwa Afrika Reviewed by Steve on Monday, November 09, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.