Kocha Kerr wa Simba anamuaminia Samatta ila tu anatakiwa afanye hiki

Baada ya mshambuliaji wa Mtanzania wa TP Mazembe, Mbwana Samatta
kuibuka mfungaji bora wa Mabingwa Afrika na timu yake kutwaa ubingwa, kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr amefunguka kuwa straika huyo anatakiwa kucheza kwa kujiamini kuhakikisha anaibeba Stars dhidi ya Algeria Jumamosi.
Kerr alisema kuwa Samatta ni moja kati ya wachezaji wenye vipaji na uwezo wa kufanya vizuri zaidi na amefanikiwa kumshuhudia akiitumikia timu ya taifa hapa nchini hivyo akishirikiana vyema na wenzake anaweza kuifikisha mbali Stars.

Akiwa Afrika Kusini Kerr amesema mshambuliaji huyo anatakiwa kujituma kwa bidii akishirikiana na wenzake ili kuweza kuandika historia nzuri zaidi kwa Waarabu hao.
“Samatta nimeona uwezo wake kupitia mechi za timu ya taifa ya hapa Tanzania lakini ni moja ya vipaji ambavyo nchi hii inatakiwa kujivunia pia kutokana na kufanya vyema akiwa na klabu yake ya TP Mazembe sasa ni wakati wa kuonyesha kweli anaweza kwa kuiongoza Stars dhidi ya Algeria akishirikiana na wenzake.
“Cha msingi anatakiwa kujiamini na ajitume uwanjani atafanikiwa na kuweza kufika mbali zaidi ya hapo alipo sasa hasa kipindi hiki ambacho anajukumu zito kuisaidia timu yake ya taifa,”alisema Kerr.
Kocha Kerr wa Simba anamuaminia Samatta ila tu anatakiwa afanye hiki
Reviewed by Steve
on
Wednesday, November 11, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, November 11, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment