Wenger: Sanchez amechoka

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kua amekua akimhitaji
sana Alexis Sanchez mpaka anachoka.
Bosi huyo Mfaransa amesema mchezaji wake huyo anahitaji kupumzika kufuatia perfomance yaka kwenye mechi ya klabu bingwa jana usiku dhidi ya Bayern Munich ambapo Gunners walishinda 2-0.
Sanchez ambaye alijiunga na Arsenal akitokea Barcelona mwaka jana, amefunga magoli 10 kwa klabu yake na timu ya taifa katika mechi saba zilizopita.
"Unaweza kuona jinsi alivyokua" Wenger aliwaambia waandishi " Alijisukuma vya kutosha lakini aliishia kuchoka. Alicheza mechi mbili na Chile, jumlisha na kusafiri, jumlisha na Watford, jumlisha na leo usiku (jana)- imezidi."
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Bayern umewavuta kuelekea kuingia hatua ya mtoano katika klabu bingwa.
Wenger: Sanchez amechoka
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 21, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment