Theo Walcott adai ujio wa Cech umeipaisha Arsenal

PETR CECH amewapeleka Arsenal kiwango kingine, hii ni kwa
mujibu wa Theo Walcott.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal hana hofu na mlinda mlango wa zamani wa Chelsea na anaamini uwepo wake, ubora na perfomance viko safi.
Cech alijiunga na Arsenal majira ya joto akitokea Chelsea kwa dau la pauni mil 10 na ameanza kuonekana kwenye michuano ya klabu bingwa jumanne iliyopita ambapo walishinda kwa 2-0 mbele ya Bayern Munich.

Hakucheza kwenye mechi zilizotangulia dhidi ya Dinamo zagreb na Olympiakos badala yake alikuepo David Ospina huku wakipoteza mechi zote mbili hali iliyowaweka katika nafasi ya chini kundini.
Lakini uwepo wa Cech dhidi ya wakali wa Ujerumani, Bayern Munich, wameweza kushinda na kuleta matumaini ambapo Walcott anaamini Cech ndio kichocheo kikubwa.
![]() |
| Moja ya mikwaju hatari aliyookoa Cech |
"Ameokoa sana katika nyakati muhimu na hicho ndicho kimeinua hali na imeonesha jinsi gani alikua katika ubora wa juu kwa miaka mingi.
"Kinachonivutia mimi ni namna nzima na jinsi anavyojiandaa kwa mchezo na jinsi anavyosaidia wengine. Ni mtu wa timu, anataka watu wafanye vizuri na ana uaminifu mkubwa kwa timu yake.
"Ndio maana alijiunga na sisi na tunashukuru kwa hilo."
Theo Walcott adai ujio wa Cech umeipaisha Arsenal
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 22, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment