Propellerads

Suarez ana kumbukumbu hii kubwa kwake kuhusu klabu bingwa Ulaya




Nyota wa FC Barcelona, Luis Suarez amefichua kumbukumbu yake
kubwa katika michuano ya klabu bingwa Ulaya (UEFA).

Myuruguay huyo ambae amecheza misimu mitatu akiwa na Liverpool amefichua kumbukumbu yake kubwa kwenye michuano ya UEFA ni ile fainali ya Liverpool na AC Milan mwaka 2005.

"Ilikua ni ndoto kubwa" Suarez aliiambia tovuti rasmi ya UEFA.

"Nakumbuka hiyo fainali. Liverpool dhidi ya Milan, ambapo Milan waliongoza 3-0 halafu Liverpool wakaja kushinda kwenye penati.

"Hiyo ndio nakumbuka sana."

Kwenye hesabu, Milan waliongoza 3-0 half time, kabla mchezo haujabadili uelekeo wake kipindi cha pili.

Magoli kutoka kwa Steven Gerard, Vladimir Smicer, na Xabi Alonso yalifanya Liverpool iwapeleke Milan kwenye penati, na hatimaye kuwashinda wataliano hao.

Suarez alijiunga na Merseyside mwaka 2011, na kufunga magoli 83 katika mechi 133 alizocheza huku akitoa mchango wake katika mashambulizi 53.
Suarez ana kumbukumbu hii kubwa kwake kuhusu klabu bingwa Ulaya Suarez ana kumbukumbu hii kubwa kwake kuhusu klabu bingwa Ulaya Reviewed by Steve on Friday, October 02, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.