Propellerads

Louis Van Gaal asema yuko tofauti na Wenger na Ferguson kwa namna hii




Bosi wa Man United, Louis Van Gaal ameeleza kua ni
namna gani yuko tofauti na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na pia aliyekua kocha mkongwe wa Man United, Sir Alex Ferguson.

Kocha huyo Mholanzi aliweka wazi mipango yake ya kutaka kustaafu ifikapo mwaka 2017 ambapo pia utakua ni mwisho wa mkataba wake, na amesema kua hayuko kama Ferguson na Wenger makocha wawili waliopata kufundisha muda mrefu zaidi Premier League, kwa hili anafikiria kuhusu changamoto zijazo.

"Ninaweka mipango na nilikua na bahati kwamba vilabu na timu za taifa zilinihitaji mimi," aliwaambia waandishi.

"Arsene Wenger na Sir Alex Ferguson nafikiri ni aina nyingine nafikiri.

"Napendelea changamoto, na wakati wote nahitaji zaidi.

"Nimepanga malengo yangu kwa kina. Ni kitu kile kile kama navyofanya sasa hivi.

"Nitastaafu. Siku zote nafanya kile nilichokisema. Nimeshapanga malengo yangu na nadhani nimeshapanga na lengo langu la mwisho pia."

VanGaal ambaye alianza kazi yake ya ukocha Uholanzi mwaka 1991, amechukua jumla ya mataji saba ya ligi akiwa na vilabu vya FC Barcelona, Bayern Munich, AZ Alkmaar na Ajax.

Mashetani wekundu Man United wanajiandaa kuumana na Arsenal katika ligi kuu jumapili hii.
Louis Van Gaal asema yuko tofauti na Wenger na Ferguson kwa namna hii Louis Van Gaal asema yuko tofauti na Wenger na Ferguson kwa namna hii Reviewed by Steve on Friday, October 02, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.