Nyota wa Arsenal adai Chelsea bado wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa

Petr Cech anaamini kua Chelsea bado wana nafasi kubwa ya
kulitetea taji la Premier League pamoja na mwanzo mbovu msimu huu.
The Blues kwa sasa wako katika nafasi ya 16 kwenye mmsimamo wa ligi wakiachwa kwa point 10 nyuma na vinara Man City.
Wamekua na mwanzo mgumu, wakipoteza mara nne na wakionekana kua na tatizo katika safu ya ulinzi.
Lakini Cech ambaye aliondoka Stamford Bridge kwenda Arsenal majira ya joto, amefunguka mshangao wake kwa matatizo ya sasa kwa klabu yake ya zamani.
"Ninashangazwa na kiwango chao kwa sababu Chelsea ni miongoni mwa vilabu bora Premier League" aliiambia tovuti moja ya nchini Czech iitwayo iDNES.
"Sipo tena pale, kwa hiyo ni ngumu kutoa tathmini kwa kinachoendelea.
"Lakini bado msimu ni mrefu na Chelsea bado ni bora kwenye macho yangu."
Nyota wa Arsenal adai Chelsea bado wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 11, 2015
Rating:



No comments:
Post a Comment