Propellerads

Hazard azungumzia wakati mgumu zaidi katika soka lake


                           
Eden Hazard ameesema kua anapitia wakati
mgumu zaidi katika soka lake.

Nyota huyo alichaguliwa kua mchezaji bora wa PFA na FWA wa mwaka msimu uliopita ambapo Chelsea walichukua Premier League na kombe la Capital One.

Hazard amekua na wakati mgumu msimu huu, akishindwa kufunga katika mechi 11.

Hali hii pia inahusiana na kiwango kisichoridhisha cha Chelsea msimu huu ambacho kimepelekea wao kua katika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi mpaka sasa.

Meneja Jose Mourinho amemwacha Hazard katika mechi kadhaa msimu huu na winga huyo sasa haelewi nini kinamsibu msimu huu.

Amesema "Huu unawezekana ukawa ni wakati mgumu zaidi katika career yangu. Kawaida kuna kupanda na kushuka . Sielewi tatizo liko wapi.

"Lakini tunajituma tuinuke.

"Kawaida inapendeza kutumia muda na timu ya taifa, na zaidi kama mambo hayaendi vizuri klabuni kwako.

"Najua ninaweza kufanya bora zaidi. Ninatakiwa kuisaidia timu ishinde."




Hazard azungumzia wakati mgumu zaidi katika soka lake Hazard azungumzia wakati mgumu zaidi katika soka lake Reviewed by Steve on Saturday, October 10, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.