Propellerads

Arsene Wenger 'hakutarajia' kua kileleni mwa ligi


                                    

Arsene Wenger amefunguka kua hakudhani endapo kikosi chake
cha Arsenal kingeweza kukaa kileleni mwa ligi baada ya mechi kumi pekee.

Arsenal walipanda hadi kileleni kufuatia ushindi wa 2-1 kwa Everton jana jumamosi, magoli kutoka kwa Olivier Giroud na Laurent Koscielny yamewafanya kushinda mechi saba kati ya kumi msimu huu.

Hata hivyo, Wenger amesema Man City kukaa juu mapema kulimpa hofu kua ingewachukua muda mrefu kufika juu na kua na matumaini makubwa na ubingwa.

Alipoulizwa kama alitarajia kua katika nafasi hiyo, aliiambia talkSPORT "Nilidhania baada ya michezo 10, hapana, kiukweli.

"Nilidhani ingechukua muda mrefu kwa sababu Man City wameanza kwa kushinda mara tano, kwa hiyo ilikua ni ngumu kufikiria kua tungerudi, lakini hamna namna. Nina furaha kwa sababu tulikua na mwanzo mgumu.

"Baada ya mchezo mgumu dhidi ya West Ham, hakuna aliyetarajia kua tungerudi juu ya msimamo baada ya mechi 10. Tupo hapo, inaonesha tumeongeza zaidi. Ni mapema sana katika msimu lakini tunashukuru hapa tulipo."
Arsene Wenger 'hakutarajia' kua kileleni mwa ligi Arsene Wenger 'hakutarajia' kua kileleni mwa ligi Reviewed by Steve on Sunday, October 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.