Propellerads

Tetesi: Barca wamtolea macho Philippe Coutinho




Imeripotiwa kua sasa Barcelona wameanza kumtolea macho
nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho.

Mbrazil huyo ambaye alijiunga Anfield akitokea Inter Milan mwaka 2013 amekua ni miongoni mwa wachezaji tegemezi katika kikosi cha kocha Brendan Rodgers siku za hivi karibuni.

Coutinho alijifunga mkataba wa muda mrefu na wakali hao wa Merseyside miezi saba iliyopita, lakini kwa mujibu wa tovuti moja ya kihispania iitwayo Fichajes, Barca wana mpango wa kumvuta nyota huyo Camp Nou.

Endapo Coutinho akiondoka, litakua ni pigo jingine kubwa kwa Liverpool kwana tayari walishawapoteza washambuliaji wao wawili , Luis Suarez aliyejiunga na Barcelona mwaka jana na Raheem Sterling aliyejiunga na Man City mwezi Julai.
Tetesi: Barca wamtolea macho Philippe Coutinho Tetesi: Barca wamtolea macho Philippe Coutinho Reviewed by Steve on Tuesday, September 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.