Propellerads

FA yamshughulikia Diego Costa




Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anakabiriwa na adhabu ya
hadi mechi tatu na chama cha soka nchini England baada ya mchezo usio wa kiuungwana kwa mlinzi wa Arsenal Laurent Koscienly katika mchezo wa jumamosi iliyopita.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kushinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, ulimalizika kwa Arsenal kuwa na wachezaji wawili pungufu waliooneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Mike Dean.

Costa ambaye anakabiliwa na adhabu kwa mchezo mbaya kwa Koscienly alioneshwa kadi ya njano na mwamuzi Mike Dean ambaye hata hivyo haikujulikana kadi hiyo ni kwa kosa la Koscienly au ni majibizano yake na Gabriel Paulista ambaye pia alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuingia katika mtego wa Costa.

FA waliipitia ripoti yenye utata ya mwamuzi Mike Dean ambaye hakumuadhibu Diego Costa kwa kitendo hicho kwa madai ya kutoona uzuri kilichotokea.

FA pia wamempa adhabu Gabriel Paulista kwa kitendo chake kilichopelekea kupigwa kadi nyekundu, wakati Saint Carzola akipewa onyo kali, na klabu zote mbili za Arsenal na Chelsea zikipigwa faini kwa kutowafunza adabu wachezaji wake. Wote wamepewa hadi saa kumi na mbili jioni jumanne hii kukata rufaa.


FA yamshughulikia Diego Costa FA yamshughulikia Diego Costa Reviewed by Steve on Tuesday, September 22, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.