Kuhusu bei aliyonunuliwa Martial, huu ndio mtazamo wa Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson amefunguka kuhusu anachofikiria juu ya
usajili wa Antony Martial majira ya joto.
Martial alikamilisha uhamisho wa thamani ya pauni mil 36 akitokea Monaco katika kipindi cha usajili ambapo wengi wamekua wakikosoa kua bei hiyo ilikua ni kubwa sana,
Lakini nyota huyo mwenye miaka 19 sasa inaonekana mambo kumnyookea Old Trafford kwani mpaka sasa amefunga magoli matatu katika michezo yake maiwili ya mwanzo.
Huku mshambuliaji mwenzake ,Wayne Rooney akionekana kua na ukame kwani katika michezo 11 iliyopita ya United hajafunga.
Akizungumza wakati akizindua kitabu chake kipya, Fergie aliulizwa kama bei ya Martial ilikua kubwa sana.
Kocha huyo mkongwe alijibu "Hapana, kuna wakati sio."
Ferguson amefunguka kwenye kitabu chake kua alifanikiwa kufundisha nyota wanne pekee ambao ni world-class katika wakati wake Man United ,Cristiano Ronaldo, Eric Cantona na Paul Scholes.
United wanatarajia kupambana na Ipswich Town kwenye michuano ya Capital One jumatano hii huku wakijiandaa tena dhidi ya Sunderland wikiendi.
Kuhusu bei aliyonunuliwa Martial, huu ndio mtazamo wa Sir Alex Ferguson
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 22, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 22, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment