Swala la kocha aliyesepa, Hanspope amesema hivi
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe
amesema kuondoka kwa kocha wao wa viungo kulikuwa kinajulikana.
Dusan Mormcilovic ameondoka nchini huku akisema Yanga itaifunga Simba.
“Unajua hili suala mnalikuza tu, Dusan alikuwa na mkataba wa miezi mitatu tu kwa ajili ya pre-season. Alipomaliza akaondoka.
“Mfano tiketi yake tokea amefika alikuwa anajua anaondoka jana, hivyo hakukuwa na kipya. Kwa sasa tumemalizana na mambo maandalizi ya mwanzo wa msimu.
“Ikiwa tutamhitaji, tutamuita tena. Hivyo hakuna ugomvi wala tatizo. Amekwenda kwao,” alisema Hans Pope.
“Maandalizi mengine yanaendelea kama kawaida na kila kitu kinakwenda vizuri. Hapa lengo ni kuwapa ndugu zetu hawa supu ya miiba.”
Swala la kocha aliyesepa, Hanspope amesema hivi
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 26, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment