Propellerads

Sir Alex Ferguson ataja nyota saba alioshindwa kuwasajili




Aliyekua kocha mkongwe wa Man United, Sir Alex Ferguson ametaja
majina ya nyota saba ambao alishindwa kuwasajili wakati wa kipindi chake Old Trafford.

Kocha huyo alizindua kitabu chake 'Leading' wiki hii ambapo ndani amegusia topic mbali mbali.

Ndani ya kitabu hicho ametaja wachezaji saba ambao baadae walikua mastaa baada ya yeye na jopo lake kushindwa kuwasajili.

Petr Cech
"Mwaka 2003 nilienda kumtizama Petr Cech golini ambapo Rennes walikua wakipambana na Auxerre. Tulidhani kua Petr ni mdogo kwa mikiki mikiki ya Premier League, lakini Petr alienda Chelsea na ndani ya muongo mmoja alifanikiwa kuokoa mikwaju ya hatari 220.

Didier Drogba
Didier Drogba nae alifatia. Alikua akiichezea  Olympique de Marseilles na tulienda kumtazama. Lakini klabu ilitaka pauni mil 25 kwa ajili yake lakini Chelsea walituwahi kabla hatujaamua."

Thomas Muller
"Thomas Muller aliyefunga magoli matano kwa Ujerumani katika finali za 2010 na 2014 kombe la dunia, alikua na umri wa miaka 10 akichezea timu ya kujitolea maili kadhaa kutoka Munich mara ya kwanza tuliposikia habari zake. Tulimwangalia na siku iliyofatia mwenyewe akajitosa Bayern Munich."

Ronaldo
"Tulitaka kumsajili mshambulia huyo mbrazil kutoka Cruzeiro mwaka 1994, lakini hatukupata ruhusa kazini ambapo alielekea PSV Eindhoven ya Uholanzi."

Sergio Aguero
"Tulikua na nafasi ya kumnunua Sergio Aguero kabla hajaenda Manchester City, lakini wakala wake alitaka bei ambayo tulikua hatujajiandaa kuilipa."

Lucas Moura
"Kuelekea mwishoni mwa wakati wangu tulikua tunamfukuzia Lucas Moura, winga wa kushoto aliye na kipaji kikubwa amaye kwa wakati huo alikua akichezea kwao Brazil klabu ya Sao Paulo. Tulitoa ofa ya pauni mil 24 kwa ajili yake, ambayo ilipanda mpaka mil 30 na tena mil 35, lakini Paris Saint-Germain walimsajili kwa pauni mil 45. David (Gill) na mimi tulikua hatujajiandaa kufikia viwango hivyo."

Raphael Varane
"2011 , nilipanda treni kutoka Euston kwenda Lille kumsainisha beki chipukizi mfaransa Raphael Varane. David Gill alikua anaelekea kukamilisha mkataba huo na Lens, ambayo ilikua ni klabu ya Varane, kabla Zinedine Zidane hajaibukia hili swala ambapo alifanikiwa kumvuta Real Madrid chini ya pua zetu. Sidhani kama Jose Mourinho aliyekua akiiongoza Real Madrid alipata nafasi ya kumuona Varane akicheza.


Sir Alex Ferguson ataja nyota saba alioshindwa kuwasajili Sir Alex Ferguson ataja nyota saba alioshindwa kuwasajili Reviewed by Steve on Thursday, September 24, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.