Mourinho alivyomshambulia tena Wenger kwa maneno
Jose Mourinho amemtupia shambulio mgomvi wake Arsene Wenger
kwa kumwambia bosi huyo wa Arsenal kua ni mtu anayependa kulaumu waamuzi na asiyekua na 'pressure'.
Mourinho ambaye kikosi chake kitaumana na Newcastle leo, hakutaja wazi jina la Wenger lakini kulikua hamna shaka nani anamuongelea pale aliposema "Kwenye hii nchi kuna meneja pekee ndio hana pressure. Wengine wote wanayo.
"Mimi nina pressure, Steve McClaren ana pressure, Manuel Pellegrini ana pressure, hata Brendan Rodgers pia. Hatuwezi kua chini ya wastani. Tunatakiwa tutimize malengo. Sina shaka na wengine, kwa sababu ni kazi ngumu. Kuna mmoja nje ya hii orodha lakini kwake ni vizuri."
Alipoulizwa anamaanisha nini, Mourinho alisema " Unajua, mtu anayeweza kuwazungumzia waamuzi kabla ya mchezo , baada ya mchezo, anaweza kuwasukuma watu eneo la ufundi, kupiga kelele, kulia asubuhi, mchana, na hakuna kinachotokea.
"Hawezi kufikia malengo yake, kufanya kazi yake, bado aendelee kua mfalme. Nimesema ni mmoja tu."
Mourinho aliongeza "Kwenye kitabu cha miongozo kinasema baadhi ya makocha wanaweza kuwazungumzia waamuzi kabla na baada ya mchezo na wengine baadhi hawawezi.
"Mimi ni miongoni mwa tulioadhibiwa kwa kuzungumzia waamuzi baada ya mchezo. Ngoja nikazie kwenye hicho kitabu cha muongozo "Unajua wengine wanaweza . Ni orodha ya kufikirika , lakini ukweli upo."
z
Mourinho alivyomshambulia tena Wenger kwa maneno
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 26, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 26, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment