Yule daktari aliyefokewa na Mourinho ameongea yake kwa mashabiki
Daktari wa Chelse Eva Carneiro amewashukuru mashabiki waliomtia
moyo baada ya kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho kuishambulia timu ya matabibu akisema kwamba ni ‘wajinga’.
Katika sare ya goli 2-2 dhidi ya Swansea kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England, Mourinho alichukizwa na kitendo cha Carneiro kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard na kutumia muda mrefu ilihali dakika zikiwa zimesalia chache.
Wakati huo Chelsea walilazimika kubaki 9 uwanjani na Swansea wakapata fursa ya kulisakama lango la Chelsea.
Mourinho alisema daktari huyo hakuelewa mchezo.
Carneiro amesema: “Napenda kuwashukuru watu wote walionipa moyo. Kiukweli nimepata faraja sana”.
Yule daktari aliyefokewa na Mourinho ameongea yake kwa mashabiki
Reviewed by Steve
on
Monday, August 10, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 10, 2015
Rating:





No comments:
Post a Comment