Propellerads

Yanga walivyoitungua Kimondo FC




Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga jana jioni ilicheza mchezo wa
kirafiki dhidid ya Kimondo Super Club ya mkoani Mbeya mchezo ambao ulikuwa ni moja ya makubaliano ya Yanga kumsajili mchezaji wa Kimondo Godfrey Mwashiuya pambano lililopigwa kwenye uwanja wa CCM uliopo wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Yanga wamnasa mwingine kutoka KMKM, ni katika kuongeza nguvu ya ushambuliaji

Kwenye mchezo huo Kimondo walikubali kipigo cha goli 4-1 ambapo mpaka mapumziko Kimondo walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 lililofungwa na Musa Salim.

Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wamebadilika na kuanza kuishushia Kimondo mvua ya magoli, Mwashiuya alifunga magoli mawili wakati Amis Tambwe na Simon Msuva kila mmoja alifunga goli moja.

Mechi hiyo ilitumiwa na Kimondo kumuaga mchezji wao Mwashiuya ambae amejunga na Yanga huku wakichukua kiasi chote cha pesa kilichotokana na viingilio vya kwenye mchezo huo.
Yanga walivyoitungua Kimondo FC Yanga walivyoitungua Kimondo FC Reviewed by Steve on Monday, August 10, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.