Van Gaal asema kua haina haja ya kuongeza nguvu mbele, hii ni kufuatia sare ya 0-0 na NewCastle
Bosi wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kua
hafikirii kuongeza mshambuliaji mwingine baada ya Wayne Rooney kutofunga mechi ya 10 mfululizo kwenye mechi ya jana dhidi ya New Castle.
Man United jana walipoteza rekodi yao ya asilimia 100 kushinda mechi za mwanzo huku tayari wakiwa na magoli matatu katika mechi tatu walizocheza.
Alipoulizwa kama anaweza kusajili mshambuliaji mpya kusaidizana na Rooney Van Gaal alijibu " Hapana kwa sababu tumekua katika kikosi kizuri mechi hizi tatu, wasi wasi wangu ni kutawala mchezo na tumefanya hivyo leo, tulifanya dhidi ya West Ham na pia Aston Villa. Tulitawala mchezo wa FC Brugges champuions League ,wa Barcelona na ule wa San Jose Earthquakes katika mechi za kujipima, sio mbaya.
"NewCastle ilikua ni moja ya michezo mizuri kwa kipindi changu.'
Pia alipoulizwa kuhusu swala la kumsajili Neymar alikanusha kwa kusema " Siwezi kusema kitu, mmekua mkiniuliza maswali kama haya kila mkutano na nimekua nikiwajibu vile vile" alimaliza kocha huyo mdachi.
Van Gaal asema kua haina haja ya kuongeza nguvu mbele, hii ni kufuatia sare ya 0-0 na NewCastle
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 23, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment