Unawajua wachezaji mwiba kwa Neymar!!?...mwenyewe amewataja
Nyota wa FC Barcelona, Neymar amefunguka wachezaji ambao
kwake yeye ni mwiba, huku watatu kati yao wakiwa ni wenzake klabuni Barca.
Mbrazil huyo alijibu baada ya kuulizwa mabeki ambao humpa wakati mgumu kukabiliana nao, ambapo alisema swali hilo ni vigumu kulijibu.
Kisha akawataja Javier Mascherano na Gerard Pique, na beki wa Brazil Thiago Silva ambao wote hupambana nao mazoezini. Mchezaji wa nne ambaye alimtaja ni Sergio Ramos.
"Ni ngumu kusema, kuna mabeki wakali wengi" aliongea katika kipindi cha FIFA Q&A.
"Mascherano, Pique, Thiago Silva, Sergio Ramos- ni mabeki wazuri"
"Kuna mabeki wengi wazuri" alimaliza.
Unawajua wachezaji mwiba kwa Neymar!!?...mwenyewe amewataja
Reviewed by Steve
on
Friday, August 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 14, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment