Unaijua sababu kubwa ya Baba Rahman kujiunga Chelsea?!!, mwenyewe afunguka
Nyota mpya aliyesajiliwa Chelsea Baba Rahman amefunguka kua
miongoni mwa sababu zilizomfanya kujiunga na Chelsea ni ushawishi mkubwa alioupata baada ya kuvutiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Michael Essien.
Kati ya mwaka 2005 hadi 2014 amecheza mechi 265 na wakali hao wa London, ambapo Rahman ameeleza kua kabla ya yote aliomba ushauri kwa nyota huyo na pia kutoka kwa mchezaji mwingine wa Chelsea Christian Atsu ambaye pia anatokea Ghana.
Rahman aliiambia tovuti rasmi ya Chelsea "Niliongea na wote wawili wakanipa mtazamo mzuri kuhusu Chelsea, waliniambia ni klabu kubwa na yenye watu wazuri sana, kitu ambacho ni kizuri kusikia.
"Nilimwangalia Essien kila nilipoweza, nilipokua Ghana kila alipocheza nilikua namwangalia, alifanya makubwa sana kwa Chelsea"
Ripoti zinadai kua Rahman ataoneka kwa mara ya kwanza kwenye mechi dhidi ya West Bromwich Albion wikiendi hii.
Unaijua sababu kubwa ya Baba Rahman kujiunga Chelsea?!!, mwenyewe afunguka
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 19, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 19, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment