Propellerads

Baada ya mechi ya jana, Man United tayari kumnasa Pedro??!





Manchester United sasa wamewashiwa taa ya kijani kumsajili
Pedro Rodriguez baada ya  FC Barcelona, mabingwa wapya wa Uefa Super Cup kuthibitisha kwamba nyota huyo ameomba kuondoka.

Barca vs Sevilla, cheki matukio katika picha hapa

United bado hawajasema ofa yao, lakini wapo tayari kulipa paundi milioni 22 ili kuvunja mkataba wa sasa wa Pedro kufuatia mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Roberto Fernandez kusema kwamba straika huyo mwenye miaka 28 jana alicheza mechi yake ya mwisho klabuni hapo.
Pedro alianzia benchi kwenye mchezo wa fainali wa UEFA Super Cup na akafunga goli la tano na la ushindi, Barca ikishinda 5-4 dhidi ya Sevilla.

Hatma ya rufaa ya kipa wa Chelsea

Manchester United wapo tayari kulipa  £22million
Kabla ya mechi kuanza hapo jana nchini Georgia, Fernandez aliiambia Televisheni ya Hispania: “Pedro ameniambia kwamba anataka kuondoka.Kwasasa hakuna ofa yoyote. Dau la kuvunja mkataba wa Pedro linazungumzika, lakini hii ni mechi yake ya mwisho”.
Manchester City pia wanahusishwa kuiwania saini ya mshambuliaji huyo wa Hispania, ila Louis van Gaal anapigana kumsajili kwa lengo la kuziba nafasi ya Angel di Maria alitetimkia PSG.
Baada ya mechi ya jana, Man United tayari kumnasa Pedro??! Baada ya mechi ya jana, Man United tayari kumnasa Pedro??! Reviewed by Steve on Wednesday, August 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.