Hatma ya rufaa ya kipa wa Chelsea
Baada ya kipa wao Thibaut Courtois kulimwa kadi nyekundu kwenye
mchezo wa ufunguzi, club ya Chelsea ilishindwa kuibuka kidedea wakiwa kwenye harakati za kutetea ubingwa wao.
Sasa club hiyo ilikata rufaa kwa ajili ya kipa wao ili afutiwe adhabu ya kukosa mechi kutokana na kadi nyekundu aliyopewa. Baada ya rufaa hiyo kupokelewa majibu ni kwamba imetupiliwa mbali.
Kwenye taarifa rasmi inasema kwamba “Malalamiko ya kutolewa nje kwa makosa inayomhusisha kipa wa Chelsea Thibaut Courtois hajafanikiwa kutokana na kamisheni inayojitegemea kuisikiliza siku ya leo. Hivyo basi kipa huyo ataendelea kutumikia adhabu yake ya kukosa michezo kadhaa.”
Thibaut Courtois alipewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Swansea kwenye dakika ya 52 baada ya kumtendea madhabi mchezaji wa Swansea.
Hatma ya rufaa ya kipa wa Chelsea
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 11, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 11, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment