Propellerads

Transfer updates: Usajili wa Schwensteiger na Di Maria.




Bosi wa Bayern munich, Pep Guardiola, amefunguka mbele ya vyombo vya habari vya Ujerumani akigusia
suala la uhamisho wa Schwensteiger na uwezekano wa kumnasa Di Maria.

SOMA: HEADLINES ZA USAJILI ZILIZOBAMBA ULAYA LEO

Di Maria, aliwahi kuripotiwa mwanzoni kabisa kua target namba moja ya wakali hao wa Bavaria, lakini kwa mujibu wa Guardiola, klabu haina mpango nae.

Pia akagusia swala la Schwensteiger, ambapo amesisitiza kua angependa kuendelea nae klabuni, lakini maamuzi yote yako kwa Schwensteiger mwenyewe.

"Nilimwambia mipango yako ya baadae unayo mwenyewe" kama alivyonukuliwa na Express.

"Basti ameweza kua na mafanikio makubwa, anaweza kuamua anachoweza kufanya mwenyewe" aliziambia ripoti.

"Bila shaka nina mpango wa kuendelea na Basti msimu ujao. lakini aamue mwenyewe"
Transfer updates: Usajili wa Schwensteiger na Di Maria. Transfer updates: Usajili wa Schwensteiger na Di Maria. Reviewed by Steve on Friday, July 03, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.