Kimondo FC wapanga kumchukulia Jerry Murro maamuzi haya..
Uongozi wa Kimondo umepanga kumfikisha Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro kwenye ‘kizimba’ cha Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
Uamuzi wa uongozi huo unatokana na madai kuwa Muro alimdhalilisha kiongozi wao.
Habari kutoka ndani ya Kimondo zimeeleza wamechukua uamuzi huo baada ya Yanga kumaliza na klabu hiyo kuhusiana na suala la usajili wa mchezaji Geofrey Mwashiuya.
“Ni kweli hatua zinachukuliwa, lakini tumeona suala hilo liende chinchini.
“Muro alimdhalilsiha sana bosi wetu, alizungumza maneno ambayo yalionyesha chuki na dharau. Huenda anadharau kwa kuwa tuko Mbozi.
“Hajui anaowadharau ni akina nani, hivyo tupe muda tukishawasilisha madai au mashitaka yetu, halafu tutazungumza rasmi,” kilieleza chanzo.
Juhudi zinafanyika kumpata Muro ili aweze kulizungumzia suala hilo ambalo linaonekana kubaki binafsi dhidi yake baada ya Yanga kumalizana na Kimondo, kivyao.
Kimondo FC wapanga kumchukulia Jerry Murro maamuzi haya..
Reviewed by Steve
on
Thursday, July 09, 2015
Rating:


