Propellerads

Huu ndo mshahara wa Messi Azam.




Stori kubwa leo hii  ni aliyekuwa winga wa Simba SC, Ramadhan Singano ‘Messi’ kusaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Azam fc, ikiwa ni siku mbili tu tangu TFF wavunje mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.
Messi amesaini mkataba mnono kwa dau la milioni 50 na atakuwa analipwa mshahara wa Milioni 2 kwa mwezi.
Kabla ya kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Simba, Wekundu wa Msimbazi walitaka winga huyo asaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 30 na mshahara wa milioni 1.5, lakini alikataa.
Huu ndo mshahara wa Messi Azam. Huu ndo mshahara wa Messi Azam. Reviewed by Steve on Thursday, July 09, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.