Vilabu 8 vyenye mashabiki wengi zaidi ulimwenguni.
Yawezekana ukawa ni mpenzi mkubwa wa soka la ulaya, hapa namaanisha ligi za Uingereza, Ujerumani, Italia, Hispania, au hata Ufaransa. Lakini yaweza ukawa hujui klabu wenye mapenzi nayo ina mashabiki wangapi!!
Leo nakuletea vilabu 8 vyenye mashabiki wengi zaidi duniani
8. Bayern Munich
Klabu hii maarufu kutoka Ujerumani inakadiriwa kua na mashabiki mil. 65 , asilimia kubwa ya mashabiki wake wako ulaya, sababu kubwa wengi kuipenda ni kutokana na mafanikio na uwezo ambapo ina mataji kibao mkononi kuanzia Ujerumani na ulaya.
7. Liverpool
Ikiwa ni klabu yenye mafanikio makubwa katika historia ya soka, Liverpool ina mashabiki wapatao mil. 70, japokua klabu imesua sua katika mwenendo wake hivi karibuni.
6. AC Milan
Ina rekodi na mafanikio makubwa katika soka, klabu hii kutoka Italia ina mashabiki wapatao mil. 99 duniani kote.
5. Chelsea
Matajiri hawa wa London wana mashabiki wapatao mil 105 , hata hivyo fan base yake inaongezeka kwa kasi zaidi. Mashabiki wake wengi wako South America, Asia na Africa.
4. Arsenal
Wengi mtashangaa kwanini Arsenal iko nafasi za juu kwenye hii orodha, lakini ndio ukweli, ikiwa na mashabiki Mil. 113. Klabu hii ina nguvu sana ya mashabiki-hata wewe ni shahidi!! mashabiki wengi wako Asia.
3. Real Madrid
Iko nafasi ya tatu katika orodha yetu ikiwa na mashabiki mil. 174. Ni klabu maarufu ambayo wachezaji wengi nyota wamepata kuichezea, pia ni klabu yenye mafanikio mafanikio. Bila shaka ni miongoni mwa klabu kubwa zaidi katika historia ya soka.
2 Barcelona
Ina mashabikio wapatao mil. 270. Ikiwa ni klabu bora duniani mara 4 pia ina mafanikio makubwa zaidi, sababu kubwa ya kupendwa na watu wengi ni mafanikio makubwa iliyo jikusanyia katika kipindi cha kuanzaia miaka ya nyuma kidogo.
1.Manchester United
Inakaa katika nafasi ya kwanza ikiwa na mashabiki mil. 354, wengi ni kutoka Asia. Bila shaka ni klabu yenye mashabiki wengi zaidi duniani.
( source: Chelsea TV)
Vilabu 8 vyenye mashabiki wengi zaidi ulimwenguni.
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 14, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, May 14, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment