Propellerads

Msuva aomba Yanga imuachie

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amerejea nchini Tanzania akitokea nchini Afrika ya Kusini alipokwenda kufanya majaribio kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
Msuva aliripotiwa kutoroka kuelekea nchini humo kufanya majaribio katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Bidvest Wits.

                                                                       
Msuva


Msuva, ambaye ameiwezesha Yanga kuwa mabingwa akiwa mfungaji bora baada ya kupashika mabao 17, ameiomba Yanga kumkubalia kujiunga na timu hiyo endapo atafuzu jaribio lake baada ya kurejea kwake siku ya jana Jumapili.
Habari zinasema kuwa mabosi wa Bidvest wameridhishwa na
mchezaji huyo na wanafungua milango ya mazungumzo na timu yake ya Yanga ili kumsajili kwa gharama yoyote.
Msuva alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea timu ya Moro United na amefunga magoli 35 katika mechi 102 alizoichezea Yanga katika michuano mbalimbali ikiwemo ya kimataifa. Endapo atajiunga na timu hiyo, atakuwa mchezaji wa pili wa Yanga kucheza Afrika ya Kusini, baada ya Mrisho Ngasa kuripotiwa kujiunga na Free State mwezi July mwaka hu
Msuva aomba Yanga imuachie Msuva aomba Yanga imuachie Reviewed by Steve on Wednesday, May 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.