Propellerads

Azam yamrejesha Stewart Hall


Taarifa kutoka  chanzo cha kuaminika ndani ya klabu ya Azam fc zinaeleza kuwa kocha wa zamani wa klabu hiyo, Muingereza Stewart John Hall anarejea tena kuwa kocha mkuu.
Hall aliyeiacha Azam fc baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2013/2014 anarejea kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu, Joseph Marius Omog

Stewart Hall


Omog alifukuzwa kazi mwezi februari mwaka huu baada ya Azam kutolewa ligi ya mabingwa Afrika  na El Merreick kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2 na nafasi yake ikachukuliwa kwa muda na aliyekuwa
kocha msaidizi, George ‘Best’ Nsimbe.
Kwasasa Nsimbe ndiye kocha mkuu wa muda na msaidizi wake ni Dennis Kitambi, hivyo kurejea kwa Hall kuna maanisha kocha mmoja anaweza kuwa msaidizi wake.
Nsimbe ameshindwa kutetea ubingwa aliochukua Omog msimu uliopita.
Azam yamrejesha Stewart Hall Azam yamrejesha Stewart Hall Reviewed by Steve on Wednesday, May 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.