Propellerads

Bayern vs Barcelona preview

Bayern Munich wana kibarua kigumu leo kuhakikisha wanasonga mbele fainali za UEFA, hata hivyo matumaini sio makubwa sana kufuatia kipigo cha mabao 3-0 mechi iliyopita pale Camp Nou dhidi ya Barcelona.

Mabao mawili yaliyofungwa na Messi na moja la Neymar yanawaweka katika njia panda ya kuendelea na michuano hii.

Matokeo yaliyopita yanamuumiza
kichwa Pep Guardiola ni mbinu gani zitakazomsaidia kupenya lango gumu la Barca na vile vile kudhibiti mashambulizi ya Barca.

Bayern wamekua na historia ya kubadilisha matokeo katika mechi za marudiano-kumbuka mechi dhidi ya Porto ambapo walipigwa 3-1 mwanzoni lakini walitoa kipigo cha mabao 6-1 mechi ya marudiano, pia waliwachapa Shakhtar Donetsk 7-0 baada ya kutoka nao droo mechi ya kwanza, kwa hiyo Bayern wana uwezo wa kushinda mabao mengi-lakini haya wataweza kuyafanya kwa Barca!!

Bila shaka Bayern safari hii wamekutana na wapinzani wenye nguvu na washambuliaji hatari kama vile Lionel Messi, Syarez na Neymar.

                                                       

Hata hivyo historia haiko upande wa Bayern kwani hamna klabu iliyowahi kusonga mechi ya marudiano kwa kipigo cha mabao kuanzia matatu , iliwahi kutokea mara moja tu ambapo Deportivo waliwapiga AC Milan 4-0 ambapo mechi ya kwanza Milan walishinda 4-1 San Siro.

Team news
Bado upande wa Bayern itawakosa Frank Ribery, Arjen Robben, David Alaba, Sebastien Rode, Holger Badstuber, ambao ni majeruhi.

Sasa ni yetu maccho pale Allianz Arena, Je Bayern watafanya maajabu!!, 
Bayern vs Barcelona preview Bayern vs Barcelona preview Reviewed by Steve on Tuesday, May 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.