Unamkubali Rashford!, sasa Van Persie ana hili la kusema
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, mshambuliaji
Robin Van Persie amempaisha Marcus Rashford kama mchezaji mwenye umuhimu wake maalum.
Rashford alikua timu ya vijana ya Man United kipindi ambacho Van Persie alikua akikipiga kwa wakali hao wa Premier League msimu wa 2012/13.
Kwa sasa Van Persie ambaye anakipiga Fenerbahce amemsifia Rashford ambapo anaamini atakua na kiwango kizuri sana Old Trafford.
"Marcus ni kama mchezaji maalum sana kwangu. Ana kitu muhimu sana," Van Persie aliiambia tovuti rasmi ya Man United "Anacheza na moyo na mbinu nzuri, daima macho yake yanaangalia golini. Mchezaji mzuri sana na atakua na hatma nzuri sana."
Unamkubali Rashford!, sasa Van Persie ana hili la kusema
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 08, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, October 08, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment