Kuhusu kushuka kiwango chake Manchester United, Rooney azungumza
Kapteni wa Manchester United, Wayne Rooney amefunguka
kwamba anastahili kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza.
Nyota huyo amekua akiachwa kwenye kikosi kinachoanza katika mechi tatu zilizopita baada ya kukosolewa kuhusu kiwango chake baada ya kupigwa 3-1 na Watford.
Rooney amesisitiza kwamba anayaelewa maamuzi ya Mourinho na yupo tayari kuvumilia na kujipanga kurejea tena kwenye kikosi cha kwanza.
"[Mourinho na mimi] tunazungumza kila siku. Nimeshasema kabla. Ninajua mchezo wa Watford sikucheza vizuri. Sikustahili kucheza mchezo uliofuata. Ninaelewa hilo n timu ilifanya vizuri , kwa hiyo ninatakiwa kutumia muda wangu kurejea nafasi yangu." aliwaambia waandishi.
Kuhusu kushuka kiwango chake Manchester United, Rooney azungumza
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 05, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, October 05, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment