Propellerads

Mourinho na Guardiola wazungumzia uhusiano wao kuelekea Manchester Derby kesho



Jose Mourinho na Pep Guardiola wamekwaruzana mara kadhaa katika kazi zao, hapa ni
jinsi walivyozungumza kwenye mkutano na waandishi kuhusu uhasimu wao na wanvyochukulia mchezo wa kesho.

Mameneja hao wawili wanakutana kwa mara ya 17 Jumamosi hii, na katika mechi zao nyingi hawakuwa na maelewano mazuri katika chumba cha waandishi.

Hata hivyo, kuelekea Manchester Derby yao ya kwanza, kila mmoja amemzungumzia vizuri mwenzake.

"City ni timu nzuri sana na meneja mzuri sana. Ni washindani wa taji,"
Mourinho alijibu alipoulizwa kuhusu uhasimu wake na Guardiola.

Kwa upande wa Guardiola amefichua kwamba walikutana miezi kadhaa iliyopita, na amefunguka kwamba atakubali glasi ya mvinyo kutoka kwa Mourinho endapo Mreno huyo akifata nyayo za Sir Alex Ferguson kumwalika mpinzani wake kunywa nae mvinyo baada ya mchezo.

"Ninamheshimu sana. Nitajitahidi kujifunza kutoka kwa wenzangu na kutoka kwake pia," Mpurinho alimzungumzia Mourinho.

"Miaka iliyopita Madrid na Barcelona haikua rahisi, lakini tulikutana miezi kadhaa iliyopita na kuzungumza vizuri.

"Nitakubali (glasi ya mvinyo) kama akinialika."




Mourinho na Guardiola wazungumzia uhusiano wao kuelekea Manchester Derby kesho Mourinho na Guardiola wazungumzia uhusiano wao kuelekea Manchester Derby kesho Reviewed by Steve on Friday, September 09, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.