Propellerads

Manchester United wameshinda jana lakini Mourinho hajafurahishwa na swala hili




Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amekosoa
kitendo cha mwamuzi kushindwa kutoa kadi nyekundu kwa Northampton Town kwenye mchezo wa EFL jna usiku.

Kocha huyo Mreno ambaye alikua kwenye kitimoto kufuatia kipigo ch mechi tatu mfululizo wiki iliyopita, ameshuhudia timu yake ikishinda kwa 3-1 jana usiku.

'Special one' anaamini kua United ilipaswa kucheza dhidi ya kikosi cha watu 10 kipindi cha pili baada ya  Jak McCourt kumchezea vibaya Memphis Depay.

Mwamuzi Stuart Attwell alishuhudia tukio hilo na kuamua kutoa kadi ya njano, lakini Mourinho naamini mwamuzi alifanya makosa.

"Ilikua ni vigumu kama nilivyotarajia, lakini tulitawala dakika 35 za mwanzo na dakika za mwishoni," Mourinho aliiambia Sky Sports News.

"Ningeacha kuongelea waamuzi na kusubiri wengine wazungumzie, wengine wanaona ukweli, wengine hawana maono ya ukweli. Ni hali mbaya. Lingeweza kua jeraha muhimu."


Manchester United wameshinda jana lakini Mourinho hajafurahishwa na swala hili Manchester United wameshinda jana lakini Mourinho hajafurahishwa na swala hili Reviewed by Steve on Thursday, September 22, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.