Kwa hali ya sasa ya Manchester United, Mourinho anamlaumu Van Gaal kwa hili
Jose Mourinho amepoteza michezo mitatu mfululizo kwa
mara ya kwana tangu mwaka 2002 na imeripotiwa anamlaumu kocha aliyemtangulia, Louis Van Gaal kwa yanayotokea.
Kocha huyo Mreno alianza kibarua chake Man United kwa kushinda mechi nne za mwanzo mfululizo.
Mjadala: Nini kinaigharimu Man United!?
Ulikua ni mwanzo mzuri kwa kocha yeyote wa Man United katika historia ya klabu hiyo, lakini kwa sasa Red Devils wamepoteza mechi tatu mfululizo.
Kwa mujibu wa machapisho tafauti tofauti ya Uingereza, Mourinho ametupa lawama zake kwa Van Gaal kutokana na mfumo wake mgumu ambao anadai umepelekea matokeo mabovu kwa klabu ambao bado unatawala akili za wachezaji wake.
"Mourinho amewaambia marafiki zake anahisi wachezaji wanatawaliwa na mfumo mgumu wa kucheza wa Van Gaal," alisema David Anderson wa Daily Mail.
Hata hivyo, Mourinho hajatoa lawama zake hadharani kwa mtangulizi wake huyo.
Mourinho na Van Gaal walipata kufanya kazi pamoja wakiwa FC Barcelona ambapo kocha Mholanzi alimfanya kocha Mreno kua msaidizi wake.
Kwa hali ya sasa ya Manchester United, Mourinho anamlaumu Van Gaal kwa hili
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 21, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, September 21, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment