Propellerads

Ivo Mapunda awananga Simba kwa hili, awasifia Jangwani



Kipa mkongwe nchini Ivo Mapunda ameamua kutoa machungu yake
kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba kuhusiana na kushindwa kumuunga mkono kipa wao Peter Manyika .



Kipa huyo wa zamani wa Yanga, Simba, Azam FC ametupia maneno yake kuonyesha hisia zake kwenye mtandao wa kijamii akisisitiza na kukemea.


Peter ambaye ni mtoto wa kipa mkongwe wa zamani wa Yanga, Mtibwa Sugar na Taifa Stars, Manyika Peter, alifiwa na babu yake ambaye ni baba wa kipa huyo wa zamani mkongwe.

Kwa mujibu wa Ivo Mapunda, amesema ameshangazwa kuona hakuna kiongozi, mchezaji au hata shabiki maarufu aliyejitokeza kumuunga mkono Peter ambaye alikuwa amevaa jezi za Simba full siku ya msiba.


Manyika, ameusifia uongozi wa Yanga kuonyesha ushirikiano mkubwa wakati wa msiba wa baba wa kipa Deugratius Munishi huku akimpongeza Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alijitokeza hadi kanisani siku hiyo kuungana na Dida na ndugu zake, marafiki pamoja na Wanayanga wengine waliojitokeza.



Ivo amekwenda mbali zaidi hadi kufikia kukumbushia viongozi wa Simba kushindwa kujitokeza msibani alipofiwa na wazazi wake wote kwa nyakati tofauti wakati akiitumikia timu hiyo.

Ivo Mapunda awananga Simba kwa hili, awasifia Jangwani Ivo Mapunda awananga Simba kwa hili, awasifia Jangwani Reviewed by Steve on Tuesday, September 06, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.