Arsenal kumsajili kinda kutoka Udinese
Imeripotiwa kwamba Arsenal wameonesha nia ya kumsajili
kinda kutoka Udinese Panos Armenakas.
Kinda huyo aliichezea Watford kwa miaka miwili kati ya 2012 na 2014 kabla hajasaini mkataba wa miaka mitatu na Udinese majira ya joto 2014.
Novemba mwaka jana, dogo huyo aliongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja zaidi, lakini bado hajapata uhakika wa kua kikosi cha kwanza.
Kwa mujibu wa Tuttomercatoweb.com, bosi wa Arsenal, Arsene Wenger ameonekana kuvutiwa na mchezaji huyo na huenda akafanya biashara dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Arsenal kumsajili kinda kutoka Udinese
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 20, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 20, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment