Propellerads

Umeipata hii ya wanasoka wa kiafrika na ushirikina huko Ulaya!!




Gazeti kubwa la The Sun limeandika article ya kiuchunguzi
kuhusu wachezaji wa EPL kujihusisha na imani za kishirikina ili kupata mafanikio uwanjani. Article hiyo ambayo imepata umaarufu mkubwa imehusisha mmoja ya wake za wachezaji licha ya kutotaja jina lake.

Mwandishi wa article hiyo anasema,“Nawajua wachezaji ambao wanajihusisha na mambo ya kishirikana. Wanaweza kupata mafanikio ya muda mfupi kutokana na imani wanayoipata na kulipa pesa nyingi sana”

Mwanamke mmoja aliyetambulishwa kuwa ni mke wa mchezaji wa EPL alisema hivi ,“Kwa baadhi ya wachezaji wa ki-africa, waganga wa kienyeji ni muhimu kwao kuliko hata manager wa timu. Kama wakiambiwa na waganga wa kienyeji waache kucheza soka leo wanaweza kuacha kweli.Mume wangu anaenda mara nyingi kijijini kwao kwa ajili ya huduma za waganga wak kienyeji, utakuta mganga analipwa pesa nyingi anaendesha magari ya kifahari na kuishi kwenye nyumba nzuri. Hao mara nyingi huwa ni waongo lakini wale wa ukweli wanaishi kwenye umaskini kibanda kimoja na hana hata huduma ya maji.”

Akiendelea kusema hivyo aliongeza pia,“Wachezaji wanaweza wasijue kama wenzao wanatumia juju lakini managers watakua wanajiuliza sana kwanini wachezaji hao wanawaomba sana ruhusu ghafla ghafla, ukiona hivyo ujue juju man kapiga simu”

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na Twitter @Kandanda 24
Umeipata hii ya wanasoka wa kiafrika na ushirikina huko Ulaya!! Umeipata hii ya wanasoka wa kiafrika na ushirikina huko Ulaya!! Reviewed by Steve on Monday, September 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.