Propellerads

Kapombe kuanza ligi akiwa jukwaani



Azam FC leo Jumamosi inaanza harakati za kusaka ubingwa
wa Ligi Kuu Bara lakini ina pigo la kuwakosa nyota wake wawili, Shomari Kapombe na Michael Bolou.

Wachezaji hao watakuwa jukwaani katika uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam wakiishuhudia timu yao ikicheza dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Kwa mujibu wa Daktari wa Azam, Twalib Misuli, Kapombe aliumia kifundo cha mguu juzi Alhamisi wakiwa katika maandalizi ya mchezo huo na Prisons wakati Bolou yeye tatizo lake la goti ni la muda mrefu.
“Kapombe bado hali yake haijawa katika hali ya ushindani, kwani ameumia mguu wa kulia na hataweza kucheza, tunaogopa kulazimisha acheze kwa kuwa anaweza kuumia zaidi.

“Huyu Bolou yupo katika programu maalum kuhusu goti lake na ataendelea kuwa chini ya uangalizi kwa muda hadi atakapokuwa vizuri kabisa ila atarejea uwanjani hivi karibuni tu,” alisema Misuli.

Kapombe aliisaidia Azam kwa kiasi kikubwa katika michuano ya Kombe la Kagame na kuiwezesha kutwaa ubingwa bila kuruhusu hata bao moja katika wavu wake.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24


Kapombe kuanza ligi akiwa jukwaani Kapombe kuanza ligi akiwa jukwaani Reviewed by Steve on Saturday, September 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.