Eti Maguli nae ajifananisha na Di Maria kwa Man United
Mshambuliaji Elius Maguli ambaye kwa sasa anakipiga Stand United ya
Shinyanga, amefunguka ya moyoni kuwa kushindwa kwake maisha ya Simba ilikuwa ni suala la kimbinu kama ambavyo wachezaji wengi wakubwa wanavyoshindwa katika baadhi ya timu licha ya kuwa na uwezo mkubwa.
Maguli amesema kuwa kocha wake wa sasa, Patrick Liewig, anamwamini na anampa nafasi ya kujiamini zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa Kocha wa Simba, Dylan Kerr.
Amesema kuwa hata Angel Di Maria alishindwa mbinu za Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal, ndiyo maana akahama kwenda PSG lakini haina maana kuwa ni mchezaji mbaya.
Maguli ambaye aliachwa Simba licha ya kufunga mabao manne katika mechi za kirafiki, amesema kuwa kwa sasa amekuwa akijiamini kwa kuwa kocha wake anamwamini pia na amempa nafasi.
“Yaani huku sina presha. Bahati nzuri hata kocha mwenyewe ameonekana kunikubali, katika kila mfumo wake nimekuwa nikisimama katika nafasi yangu kama fowadi wa mwisho. Anayo mifumo mingi lakini huwa sibadilishwi nafasi, ukweli ni kuwa tunaelewana vizuri,” alisema.
Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Eti Maguli nae ajifananisha na Di Maria kwa Man United
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 12, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment