Propellerads

Kwanini wachezaji wengi wa Simba hawakuwemo kikosi cha Stars, Kibadaeni afunguka kiivi



Mshauri wa Benchi la Ufundi la Taifa Stars, Abdallah Kibadeni
ambaye kitaaluma ni kocha, ametaja sababu ya wachezaji wa Klabu ya Simba kutopata nafasi kubwa katika kikosi cha kwanza cha Stars katika mechi dhidi ya Nigeria.

Kibadeni amejitokeza kufunguka juu ya suala hilo ambalo limekuwa likizungumzwa mitaani kutokana na kikosi cha Stars kukosa mchezaji wa Simba katika 11 walioanza kwenye mchezo huo wa Jumamosi iliyopita.

 Kibadeni ambaye ni gwiji wa Simba amesema hawakupanga kikosi kwa kuangalia majina ya timu, bali uwezo wa mchezaji na aina ya mbinu walizozipanga.

“Tulitumia akili ya kisayansi kukipanga kikosi hicho kutokana na kutojua falsafa na mbinu za kocha mkuu mpya wa Nigeria, Sunday Oliseh. Tuliamua kuwapanga kutokana na jinsi walivyozoeana kwa muda mrefu, mfano Barthez (Ally Mustapha), Cannavaro (Nadir Haroub), Yondani (Kelvin) na Haji Mwinyi wamekuwa wakicheza pamoja na kwa kuelewana.

“Viungo Himid (Mao), Mudathir (Yahya), Farid (Mussa) na beki wa pembeni Kapombe (Shomari) nao wamekuwa na maelewano mazuri kuanzia ngazi ya klabu na hata tulivyokuwa kambini.

“Katika safu ya ushambuliaji Samatta (Mbwana), Ulimwengu (Thomas) wote wapo TP Mazembe wanajuana vizuri. Tulimuongeza Ngassa (Mrisho) kwa kuwa ni mzoefu na uwezo wake unajulikana.


“Hivyo hakukuwa na lengo baya kwa wachezaji wa Simba na wala hawatakiwi kulalamika, ndiyo maana uliona alivyoingia Ndemla (Said) naye alicheza vizuri kwa kuwa alikuwa ameshausoma mchezo. Tuache lawana na tuwapongeze vijana kwa kazi nzuri,” alisema Kibadeni.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Kwanini wachezaji wengi wa Simba hawakuwemo kikosi cha Stars, Kibadaeni afunguka kiivi Kwanini wachezaji wengi wa Simba hawakuwemo kikosi cha Stars, Kibadaeni afunguka kiivi Reviewed by Steve on Saturday, September 12, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.