Wenger nae ajibu kauli ya Mourinho
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amemjibu Mourinho ambae amedai kua waliiacha
falsafa yao ya ushambuliaji na kulinda goli moja.
The Gunners walikua wakilinda zaidi katika kipindi cha pili katika mechi hiyo baada ya bao la Chamberlain katika kipindi cha kwanza.
Bao hillo lilitosha kuivunja rekodi ya Mourinho ya kutofungwa na Wenger katika mechi 13 zilizopita, ambapo kocha wa Chelsea anadai waliuacha uchezaji wao na kulinda goli ili washinde.
Hata hivyo, Wenger amefunguka kua staili yao ya uchezaji haikupania kutetea bao hilo moja pekee ila walicheza kwa umoja.
"Hatujaacha kitu. Tulilinda vizuri. Timu yetu imejiegemeza katika umoja, ushirikiano na kulinda na pia kushambulia vizuri" aliiambia tovuti rasmi ya Arsenal.
"Hatukuvuruga falsafa yetu ila tulitaka kushinda mchezo huu"
Arsenal wataanza Premier League kwa kuwakaribisha West Ham Jumapili ijayo.
Wenger nae ajibu kauli ya Mourinho
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment