Maneno ya Mourinho baada ya kupoteza dhidi ya Arsenal
Bosi wa Chelsea baada ya kupoteza mechi ya jana dhidi amedai kua Arsenal waliiacha
falsafa yao ya ushambuliaji na kulinda bao lao moja lakini amewapongeza kwa ushindi katika mechi hiyo ya ngao ya jamii.
Mourinho anasema kua anaamini kua kua kikosi chake kilikua ni 'best team' katika mechi hiyo iliyopigwa Wembley.
Alex-Oxlade Chamberlain aliipatia Arsenal bao katika kipindi cha kwanza, huku Chelsea wakipoteza nafasi nyingi kupitia Ramires na Hazard.
Mourinho aliwaambia BT Sport " Tulikua ni timu bora. Tulikua na hamasa zaidi, tulimiliki mpira zaidi mchezoni"
"Lakini timu inapokua nyuma, nguvu ya kurudisha magoli inakua vigumu kwa sababu atu wanakua hawapo sharp"
"Arsenal walilinda goli watu kumi, lakini kila mmoja alikua na mpangilio mzuri...hongera kwao"
Pia Mourinho aliongezea kua kushinda Premier League ni kazi pevu kwake, lakini pia itakua ngumu kwa kila mmoja.
Maneno ya Mourinho baada ya kupoteza dhidi ya Arsenal
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment