Propellerads

Wenger alisusa kumpa mkono Mourinho, unajua kwanini!!...mwenyewe aeleza




Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kua ukosefu wa
heshima wa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ndio ulisababisha yeye aamue 'kupotezea' kumpa mkono Mourinho kwenye mechi ya jana ngao ya jamii.



Kwenye mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Arsenal kushinda kwa goli moja pekee, Wenger aliondoa uteja wa kufungwa na Mourinho katika mechi 13 zilizopita.

Baada ya mechi Mourinho alionekana akiwapongeza wachezaji wa Arsenal lakini Wenger alimpita kwa nyuma na kuondoka, hali iliyoashiria uhasama wao wa muda mrefu hauko karibu kuisha.

"Nilishikana mikono na watu wachache baada ya mchezo, lakini hakukua na kitu cha kueleweka pale"  Wenger aliiambia Irish Times

"Ninaamini katika kazi ambapo unatakiwa uwe na heshima na umuheshimu kila mtu" alimaliza Wenger.

Mourinho nae kwa upande wake alifunguka " Ukiangalia picha, utaona nilipokua. Nilikua nawasubiria washindi kama uliamua kuniruka uliniruka tu.

"Kila mchezaji wa Arsenal alikuja upande wangu, kitu ambacho kilikua rahisi zaidi kufanya.

"Kama watu wengine hawakuja upande wangu, sio tatizo, sio story, huo sio mwisho wa dunia"



Wenger alisusa kumpa mkono Mourinho, unajua kwanini!!...mwenyewe aeleza Wenger alisusa kumpa mkono Mourinho, unajua kwanini!!...mwenyewe aeleza Reviewed by Steve on Monday, August 03, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.