Maoni ya Cannavaro juu ya Zuttah
Beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameibuka na kusema kuwa beki wa pembeni wa timu hiyo,
Joseph Zuttah, anahitaji kupewa muda ili aweze kuenda sawa na timu hiyo.
Zuttah, raia wa Ghana, alionyesha kiwango kidogo katika michuano ya Kombe la Kagame kiasi cha kuwafanya mashabiki wamchukie na kumjadili kila kona.
Cannavaro ambaye ni nahodha wa Yanga, amesema kuwa ni vigumu kwa upande wake kumjaji mchezaji kwa muda mfupi na kudai kuwa anachoamini yeye, mchezaji huyo ni mzuri lakini anahitaji muda ili aweze kufiti na wenzake.
“Kwa upande wangu, Zuttah namuona ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo, lakini ni vigumu kuweza kumjaji mtu kwa mechi chache tu alizocheza.
‘Bado anahitaji muda wa kuweza kuwa vizuri baada ya kuzoeana na wenzake, lakini kwa upande wangu, namuona ni mchezaji mzuri na hana shida yoyote,” alisema Cannavaro.
Maoni ya Cannavaro juu ya Zuttah
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 03, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment