Propellerads

Uhamisho wa Benzema ulipofikia, pia John Stones, hizo na nyigine ingia hapa upate kufaham




Usajili Ulaya kwa sasa umeshika kasi sana, kwani kwa sasa msimu mpya wa
ligi mbali mbali umekaribia kuanza rasmi.

Hapa nakuletea story mbali mbali za usajili zilizotawala vichwa vya magazeti England leo jumatatu

Arsenal sasa huru kumsajili Benzema.
Kulingana na ripoti, Arsenal sasa wanaweza kumnunua nyota KIarim Benzema kwani tayari Real Madrid wametangaza kumuuza nyota huyo.

Roberto Martinez bado anamuhitaji John Stones
Kocha  wa Everton, Roberto Martinez amesisitiza kua beki John Stones ataendelea kuwepo Goodson Park pamoja na kuhusishwa sana na klabu ya Chelsea.

Man City wakubaliana dili la Dzeko
Manchester City wamekubaliana dili la kumuuza nyota wake Edin Dzeko kwa klabu ya Roma, dau lina thamani ya £14m.

Man United wamuongezea Ashley Young mkataba
Ashley Young yuko karibu kusaini mkataba mwingine mpya wa miaka mitatu kuendelea kukipiga Old Trafford.

Rio Ferdinand "Cech ni uhamisho mzuri zaidi msimu huu"
Beki wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand amesifia kua usajili wa Petr Cech kwenda Arsenal akitokea Chelsea kua ni usajili ambao The gunners walilamba dume.

Arsenal kuongeza mkataba wa Nacho Monreal
Arsenal kwa sasa wana mpango wa kuongeza mkataba mwingine na beki wake Nacho Monreal kwa mujibu wa ripoti.

Arsenal kumtengea Benzema  £46m
Kwa mujibu wa ripoti, Arsenal wamejipanga kumchukua Karim Benzema kwa dau la pauni 46m kutoka Real Madrid.

Baba Rahman kufanya vipimo vya afya Chelsea
Beki wa Augsburg, Baba Rahman anatarajiwa kutua London siku chache zijazo ili kufanya vipimo vya afya Stamford Bridge.

Rafael akaribia kuhamia Lyon
Beki wa Man United, Rafael amekaribia kutimkia Lyon ya Ufaransa kwani sasa yuko hatua za mwisho, Rafael ameshindwa kupata namba ya kudumu kikosi cha kwanza chini ya kocha Louis van Gaal
Uhamisho wa Benzema ulipofikia, pia John Stones, hizo na nyigine ingia hapa upate kufaham Uhamisho wa Benzema ulipofikia, pia John Stones, hizo na nyigine ingia hapa upate kufaham Reviewed by Steve on Monday, August 03, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.