Uzi mpya wa Man United na rekodi waliyovunja vipo hapa
Manchester United imekuwa miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha jei zao zitakazotumiwa kwa
ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja rekodi kwa kuwa ni klabu inayopiga pesa nyingi duniani kutoka kwa watengezaji wa jezi ambapo jezi zao zitakuwa zikitengenezwa na kampuni ya Adidas baada ya kusaini dili la pauni milioni 750.
Kabla ya Adidas Nike ndio walikuwa watengenezaji wa jezi za mashetani wekundu na wamedumu kwa muda wa miaka 13 kabla ya Adidas kuchukua dili hilo baada ya mkataba wa Nike na Man U kumalizika.
Wakongwe hao (Adidas) wa kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wnaweza kutengeneza kiasi cha pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man U kwa muda wa miaka 10 ijayo.
Dili hilo kati ya Manchester United na Adidas linayapiku madili mengine ya klabu ambazo zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
Jezi hizo mpya zitakuwa na muonekano kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V yenye rangi nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake.
Uzi mpya wa Man United na rekodi waliyovunja vipo hapa
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 02, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 02, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment