Tetesi za usajili Ulaya leo Ijumaa.
Katika tetesi za usajili leo kuna zile zilizokamata sana vichwa vya magazeti Ulaya, na hizi zinawahusu nyota
kama vile Angel Di Maria, Isco, Nicolas Otamendi, Fernando Llorente, Victor Valdes na Sami Khedira.
PSG wanajiamini kumnasa Di Maria
Paris Saint-Germany wamedaiwa kujiamini kua wanaweza kumsainisha nyota Angel Di Maria ndani ya wiki hii, pia inasemekana Di Maria mwenyewe tayari ameshafanya mazungumzo binafsi na mabingwa hao wa Ufaransa lakini kilichobaki ni makubaliano ya ada ya uhamisho kati ya Red devils na PSG.
Juve wanamfukuzia Isco
Nyota wa Real Madrid, Isco anaonekana kua target kubwa ya Juve kwa sasa. Kufuatia kutimka kwa Carlos Tevez, Andrea Pirlo vilevile Artulo Vidal nae yuko mbioni kutimkia Bayern Munich, hivyo Juve wanataka kumnasa Isco kama kiungo wao mpya.
Otamendi anakaribia kujiunga Man United
Nyota wa Valencia, Nicolas Otamendi hakuwepo wakati klabu ikizindua uzi wake mpya kwa msimu huu, hali iliyozidi kukoleza taarifa za yeye kujiunga Old Traford, Chelsea nao walidaiwa kuingilia dili lakini imekua ngumu kwani nyota huyo inaonekana yuko kwenye hatua za mwisho sana kujiunga na Red Devils.
Real na Porto wanachuana kwa Llorente
Inadaiwa Real madrid na Porto wako katika kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente. Los Blancos wanatafuta mbadala wa Karim Benzema, huku Porto nao wakitafuta pia mrithi wa Jackson Martinez .
Valencia wanammendea Valdes
Valencia wameripotiwa kua katika uhitji mkubwa wa golikipa, na kwa sasa inaonekana kipa wa Man United, Victor Valdes ndio lengo lao kubwa. Mkali huyo yuko katika harakati za kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya kocha Van Gaal kutangaza kua klabu haina mpango nae.
Kwingineko
Nyota wa Ujerumani, Sami Khedira amejiunga na Juventus wiki hii kwa uhamisho huru akitokea Real madrid, Huku Sunderland nao wakitangaza kumnasa Younes Kaboul kutokea Tottenham kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni mil 3.5, Yaya sanogo wa Arsenal nae amejiunga Ajax kwa mkopo wa muda mrefu.
Tetesi za usajili Ulaya leo Ijumaa.
Reviewed by Steve
on
Friday, July 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 17, 2015
Rating:
