Mancini afunguka kwa nini anamuonea wivu Mourinho
Bosi wa Inter, Roberto Mancini amefunguka kwanini anamuonea wivu hasimu wake wa
muda mrefu, Jose Mourinho.
Mancini ameeleza hisia zake kuhusu Mourinho baada ya kocha huyo Mreno kushinda mataji matatu msimu mmoja baada ya yeye kutimuliwa.
"Sikutegemea kufukuzwa" Mancini aliiambia Gazetta Tv
"(Massimo) Moratti aliniita na kuniambia amechukua maamuzi hayo.
"Nina wivu kuhusiana na treble(mataji matatu)? Hizo ni hisia za kawaida, lakini naamini mambo yanatokea kwa sababu yalipangwa kutokea"
Mancini ambaye alirejea tena Inter kwa kipindi kingine cha pili, anajitahidi kuirudisha timu katika kuchukua ubingwa kama zamani.
"Yote kwa yote, sikutarajia kama ningerudi Inter" aliongeza.
Mancini akiwa na Inter amepata kushinda mataji matatu ya Serie A, mawili ya Coppa Italia na moja la Supercoppa Italia, huku Mourinho akiwa Inter amechukua mawili ya Serie A, Coppa Italia moja, na Champions League.
Mancini afunguka kwa nini anamuonea wivu Mourinho
Reviewed by Steve
on
Friday, July 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, July 17, 2015
Rating:
